ZEPHANIA LIFE HERBAL CLINIC
  • Home
  • FAQ
  • About
  • Blog
  • Contact
  • Home
  • FAQ
  • About
  • Blog
  • Contact
Picture

TUNATIBU TATIZO LA NGUVU ZA KIUME HADI KUPONA KABISA
_____________________________________

SIMU: +255 766 431 675/+255 656 620 725 
EMAIL: 
khamisiibra@gmail.com

Tiba ya kifafa

​Kifafa kwa Kiingereza hutwa Epilepsy. Huu ni ugongwa wa ubongo unaosababishwa na hitilifu ya kiumeme katika seli za ubongo.  Kama tunavyojua ndani ya miili yetu kuna umeme. Umeme huu wa mwilini ni kama umeme ulio katika majumba yetu. Ikitokea shida yoyote ya kiumeme kunakuwa na tatizo.
 
Kadhalika katika ubongo ambao unaendeshwa kiumeme, ikitokea shida yoyote ya kiumeme basi hapo kunapatikaana tatizo ambalo tunaita kwa Kiswahili Kifafa na kwa Kiingereza huitwa Epilepsy. Kuhusika na kifafa ni kwamba, kunapokuwa na utendaji usio wa kawaida katika chembe hai za ubongo, basi hapo mtu huzimia. Wanasayansi na watafiti duniani bado hawajui kwa nini kunatokea utendaji mbaya wa chembe za ubongo.
 
Kwa nini umeme unaleta matatizo katika ubongo? Ubongo wa binadamu una mabilioni ya seli za neva. Seli hizi zinafanya kazi kwa ushirikano mkubwa sana kila moja kupitia chaji ndogo ndogo za umeme ambazo huwaka na kuzima. Wakati baadhi ya ama hizi seli zote kwa ghafla huanza kuwaka kwa pamoja, wimbi la nguvu za umeme hupita kwenye ubongo na husababisha kifafa ama kuzirai.Kifafa hiki huweza kutambulika kwa dalili zifuatazo:

  • Kuona maluwe luwe (aura)
  • Kupoteza fahamu/kupoteza akili
  • Kuanguka na kutupa tupa miguu au mikono
  • Kukaza mdomo
  • Kutoa povu na huwa inamalizia na kutoa haja ndogo au kubwa wakati mwingine

Je, kifafa huambukiza?
 
Baadhi ya wasomaji wamekuwa wakiuliza swali hili. Kwa hakika ni hapana. Zaidi, kifafa hutokana na urithi, na sio ugonjwa wa kuambukiza kamwe. Urithi maana yake ni kwamba ugonjwa huu unaweza kuwa umeurithi kwa wazazi wote wawili au mzazi mmoja. Pia, kifafa huweza kusababishwa na ajali. Kama wakati wa ajali ubongo uliathirika basi unaweza kupata kifafa. Kwa watu wenye ugonjwa wa kiharusi ambao kwa Kiingereza huitwa Stroke, hawa nao wanaweza kupata kifafa. Lakini pia mtu anaweza kudhurika wakati wa kuzaliwa na hivyo ikampelekea kupata kifafa.
 
Matibabu ya kifafa
Kwa hospitali kifafa hakitibiki isipokuwa kuna dawa za kutuliza makali ya kifafa au kukifanya kisiwe kinajirudia mara kwa mara sana. Na dawa hizi zinapaswa kutumiwa muda wote wa maisha. Na mgonjwa anapaswa kuhudhuria kliniki maalumu kwa ajili ya tatizo hili kwa ajili ya kuangalia maendeleo yake, au pale anapoona kuna tatizo.
 
Tahadhari kwa mgonjwa wa kifafa
Desturi ya kifafa ni kwamba huwa kinatokea ghafla. Kwa mtu ambaye yuko karibu na mgonjwa wa kifafa anapaswa atoe vitu vyote vya hatari kwa sababu wakati huu mgonjwa anakuwa fahamu zimempotea. Hivyo anaweza kujijeruhi vibaya sana na hata kumsababishia kifo.
 
Kwa hakika, wagonjwa wengi wa kifafa huwa wanaumia vibaya sana kwa sababu ya hali hii na wengine huweza kuanguka katika moto na kuungua vibaya sana. Kwa hali hii anapaswa mtu aliye karibu na mgonjwa wa kifafa aondoe haraka vitu hatari kama moto, kisu au vitu vyenye ncha kali, jiko, mawe n.k. Weka katika kitu laini baina ya kichwa chake na sakafu.
 
Baadhi ya wagonjwa wa kifafa huweza kujitambua kuwa wako karibu kuanguka kifafa, ni vizuri mgonjwa akakaa mazingira mazuri ambayo hayana vitu hatarishi.
 
Baada ya kuanguka kifafa
Mara nyingi baada ya mgonjwa kuanguka kifafa, mgonjwa anakuwa anapoteza fahamu anakuwa kama kachanganyikiwa. Hapa mgonjwa anahitaji msaada sana kutoka kwa jamaa, ndugu na marafiki. 
Picture
Dr. Khamisi Ibrahim Zephania ni daktari bingwa aliyebobea katika kutibu matatizo ya nguvu za kiume na afya ya uzazi wa mwanaume kwa ujumla. Anatibu kuanzia chanzo cha tatizo. Anatibu hadi tatizo lako liishe kabisa. Ni matatibabu ya uhakika wala siyo ya kubahatisha. Pia, anakupatia ushauri juu ya afya yako kwa ujumla na chakula kulingana na chanzo chako cha tatizo lako. Soma zaidi maana ya kupungua nguvu za kiume, sababu za kupungua nguvu za kiume na matibabu sahihi ya kutibu upungufu wa nguvu za kiume kwa usahihi na ufasaha.
Maelezo zaidi bofya hapa
Powered by Create your own unique website with customizable templates.